• HABARI MPYA

  Tuesday, November 28, 2017

  SAMATTA AENGULIWA TUZO YA MWANASOKA BORA AFRIKA

  NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Samatta ameshindwa kuingia katika orodha ya wanasoka 11 Bora wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika 2017.
  Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha mbili leo, ya wachezaji 11 wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika na wengine 10 wanaowania tuzo ya Mwanasoja Bora Anayecheza Afrika.
  Na orodha hizo mbili zinafuatia kura zilizopigwa na Wajumbe wa Kamati ya Ufundi na Maendeleo ya CAF, Jopo la Wanahabari  wa Kitengo cha Wanahabari cha CAF na vyombo vya Habari vinavyojitegemea na wataalamu wa Televisheni.
  Mbwana Samatta ameshindwa kuingia 11 Bora ya wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika 2017

  Kwa Pamoja wataalamu hao walipunguza orodha ya wawania tuzo kutoka orodha ndefu ya watu 30 ya awali, ambayo ndani yake alikuwemo Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji.
  Hatua ya pili itawahusisha makocha Wakuu wa timu za taifa au Wakurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho au Chama cha soka cha nchi husika na Wajumbe 10 kutoka Vyombo binafasi vya Habari na Waatalamu wa Televisheni.
  Kwa mara ya kwanza, Manahodha wa timu za wakubwa za wanaume pia watahusihwa kwenye zoezi hilo kutoa maamuzi.
  Sherehe za tuzo zitafanyika Alhamisi ya Januari 4, mwakanimji Accra, Ghana.
  WANAOWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA WA AFRIKA
  1.     Bertrand Traore (Burkina Faso & Olympique Lyon)          2.     Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns)  
  3.     Karim El Ahmadi (Morocco & Feyenoord)        
  4.     Keita Balde (Senegal & Monaco)                    
  5.     Mohamed Salah (Misri & Liverpool)
  6.     Naby Keita (Guinea & RB Leipzig)      
  7.     Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & B. Dortmund)
  8.     Sadio Mane (Senegal & Liverpool)       
  9.     Victor Moses (Nigeria & Chelsea)        
  10.  Vincent Aboubakar (Cameroon & Porto)           
  11.  Yacine Brahimi (Algeria & Porto)
  TUZO YA MWANASOKA BORA ANAYECHEZA AFRIKA
  1.     Achraf Bencharki (Morocco & Wydad Athletic Club)    
  2.     Ahmed Fathi (Misri & Al Ahly)
  3.     Ali Maaloul (Tunisia & Al Ahly)          
  4.     Aristide Bance (Burkina Faso & El Masry)
  5.     Ben Malango (DRC & TP Mazembe)       
  6.     Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns)
  7.     Jeremy Brockie (New Zealand & Supersport)    
  8.     Junior Ajayi (Nigeria & Al Ahly)
  9.       Mohamed Ounnajem (Morooco & Wydad Casablanca)
  10.  Taha Yassine Khenisssi (Tunisia & Esperance)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AENGULIWA TUZO YA MWANASOKA BORA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top