• HABARI MPYA

  Wednesday, November 29, 2017

  WENGER ASEMA PETR CECH ANATAKA KUZEEKEA ARSENAL

  KIPA Petr Cech hana mpango wa kuondoka Arsenal kwa mujibu wa kocha Mfaransa wa klabu hiyo, Arsene Wenger
  Wenger amesema mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 35 amepunguza uzito ili kuongeza muda wake wa kuendelea kucheza kadri iwezekanavyo.
  "Anazeeka, na wote tunazeeka,"amesema Wenger. "Lakini wakati anazeeka, pia anakuwa fiti kuliko alivyowahi kuwa,". 
  "Ameweka msistizo mwingi kwenye maandalizi. Amekuwa mwembamba kuliko alivyokuwa. Nafikiri ananufaika na hilo,".
  "Amepunguza uzito fulani. Siyo sana, kilo mbili au tatu tu. Lakini ni nyingi ikiwa unakwenda kupanda farasi, unaweka kitu nyua kuongeza uzito na farasi anakuwa mkubwa,". 
  Kocha wa Arsenal anaanza kumfananisha kipa wake huyo na mlinda mlango wa zamani wa Manchester United, Edwin Van Der Sar. 
  Petr Cech hana mpango wa kuondoka Arsenal kwa mujibu wa kocha Mfaransa wa klabu hiyo, Aesene Wenger PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Mholanzi huyo anashikilia rekodi ya mchezaji mzee zaidi kucheza Ligi Kuu ya England alipoidakia Manchester United hadi akiwa ana umri wa miaka 40 na siku 205.
  "Cech amefanya hivyo kwa sababu anajisikia vizuri na anataka kuwa bora," amesema Wenger. 
  "Petr Cech ni mtu sahihi. Na huwezi kufika alipofika yeye kama hautakuwa hivyo, wakat wote uwe katika uborsa wako,".
  "Namkumbuka Van der Sar alipokuwa Manchester United, Namfananisha naye. Ni weledi na wana maumbo yanayoshabihiana pamoja a ubora,". 
  "Na Van der Sar aliacha soka kwa sababu aliamua mwenyewe kustaafu. Kwa sababu Manchester United walimtaka aongeze mkataba wa mwaka mmoja zaidi. Sikatai hioo, lakini itategemea na kiwango chake,"amesema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WENGER ASEMA PETR CECH ANATAKA KUZEEKEA ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top