• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 26, 2017

  NI TP MAZEMBE MABINGWA KOMBE LA SHIRIKISHO 2017

  TIMU ya TP Mazembe imefanikiwa kutwaa Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) baada ya kulazimisha sare ya 0-0 na wenyeji, SuperSport United Uwanja wa Lucas Moripe mjini Tshwane.
  Mazembe inatwaa ubingwa wa Kombe hilo dogo la michunao ya klabu barani kwa ushindi wa jumla wa 2-1 ilioupata mjini Lubumbashi kwenye mchezo wa kwanza.
  Ushindi huo, unamaanisha The Ravens wamefanikiwa kutetea taji ambalo walilitwaa kwa mara ya kwanza mwaka jana.
  Pamphile Mihayo anakuwa kocha wa 10 Mwafrika kutwaa Kombe la Shirikisho la Soka Afrika ndani ya fainali 14 za michuano hiyo.
  Kocha wa SuperSports United ya Afrika Kusini, Eric Tinkler ameshindwa kutimiza ndoto za kutwaa taji la kwanza la michuano ya Afrika.
  Mkongwe wa Tunisia, Faouzi Benzarti amebeba taji hilo mara mbili akiwa na Etoile Sahel, mwaka 2006 na 2015.
  Ni kati ya makocha watatu walioshinda Kombe la Shirikisho na wakashinda pia Ligi ya Mabingwa, akipata mafanikio akiwa na klabu ya Esperance.
  Makocha wengine wawili wazawa waliotwaa mataji yote ya klabu barani AfrikaThe ni Mghana Cecil Jones Attuquayefio, aliyefariki dunia mwaka 2015 na Mmorocco Hussein Amotta. 
  Attuquayefio alishinda mataji yote akiwa na vigogo wa Accra, Hearts of Oak wakati Amotta alibeba Kombe la Shirikisho akiwa na FUS Rabat na Ligi ya Mabingwa mwaka huu akiwa na Wydad Casablanca. 
  Kikosi cha SuperSport kilikuwa: Ronwen Williams, Siyabonga Nhlapo/Grant Kekana dk46, Tefu Mashamaite, Clayton Daniels, Aubrey Modiba, Dean Furman, Reneilwe Letsholonyane, Thuso Phala, Sipho Mbule/Kingston Nkhatha dk81, Bradley Grobler na Jeremy Brockie/Dove Wome dk66.
  TP Mazembe: Sylvain Gbouhouo, Issama Mpeko, Joel Kimwaki, Chongo Kabaso, Zola Kiaku, Nathan Sinkala, Koffi Kouame, Daniel Nii Adjei/Miche Mika dk64, Adama Traore/Solomon Asante dk74, Ben Malango na Rainford Kalaba/Mechak Elia dk60.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NI TP MAZEMBE MABINGWA KOMBE LA SHIRIKISHO 2017 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top