• HABARI MPYA

  Wednesday, November 29, 2017

  HIMID MAO AWASHINDA WAGENI NA KUWA MCHEZAJI BORA WA AZAM OKOTBA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa Azam FC, Himid Mao ‘Ninja’, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa klabu kwa mwezi Oktoba baada ya kuwashinda wageni watatu, Waghana kipa Razak Abalora, beki Yakubu Mohammed na Mzimbabwe beki Bruce Kangwa pamoja na mzalendo mwenzake, Aggrey Morris.
  Mao anakuwa mchezaji wa tatu msimu huu kushinda tuzo hiyo baada ya Yakubu Mohammed aliyeshinda Agosti na mshambuliaji Mbaraka Yusuph aliyeibeba Septemba.
  Nahodha huyo msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, ametwaa tuzo hiyo baada ya kujizolea kura 320 za mashabiki zikiwa ni asilimia 47 ya kura zote 680 zilizopigwa kupitia mtandao wa poll kwenye akaunti ya facebook ya Azam FC.
  Himid Mao ‘Ninja’, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Azam FC mwezi Oktoba 

  Aidha kipa mahiri wa timu hiyo, Razak Abalora, ambaye mpaka sasa amefungwa mabao matatu kwenye mechi 11 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ameshika nafasi ya pili baada ya kujizolea kura 292 sawa na asilimia 43 za kura zote zilizopigwa.
  Beki wa kushoto, Kangwa ameshika nafasi ya nne kwa kura 41 alizojizolea (asilimia sita) huku Moris akimalizia orodha hiyo baada ya kukusanya kura 27 zikiwa ni asilimia nne za kura zote zilizopigwa na mashabiki (680).
  Tuzo hiyo inadhaminiwa na Wadhamini wakuu wa Azam FC, Benki ya NMB, ambayo kwa sasa ndio bora kabisa Tanzania ikikuhakikishia usalama wa fedha zako na ikiwa na matawi mengi yaliyosambaa kote hapa nchini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HIMID MAO AWASHINDA WAGENI NA KUWA MCHEZAJI BORA WA AZAM OKOTBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top