• HABARI MPYA

    Tuesday, July 16, 2013

    PIGO TENA MAN UNITED, FABREGAS AWATOLEA MBAVUNI TENA ILE KINOMA NOMA

    IMEWEKWA JULAI 16, 2013 SAA 9:52 ALASIRI
    KOCHA wa Manchester United, David Moyes amepata pigo lingine baada ya kiungo wa Barcelona, Cesc Fabregas kumuambia kocha wake, Tito Vilanova anataka kubaki kwa vigogo hao wa Katalunya.
    United ilithibitisha sana kutenga dau la Pauni Milioni 26 kwa ajili ya Nahodha huyo wa Arsenal.
    Harakati hizo zilikuja baada ya Thiago Alcantara kuamua kujiunga na kocha wake wa zamani, Pep Guardiola katika klabu ya Bayern Munich badala ya mabingwa hao wa England. 
    United front? Fabregas is a target for new United boss David Moyes
    United mbele? Fabregas anatakiwa na kocha mpya wa United, David Moyes

    Na sasa kocha wa Barca, Vilanova ameanza mazungumzo na Fabregas ambaye ameweka wazi anataka kubaki Nou Camp.
    Vilanova alisema: "Cesc amepata ofa kutoka klabu nyingine. Nimezungumza naye na ameniambia anataka kubaki. Ndoto zake ni kung'ara hapa.
    Habari njema zaidi kwa mashabiki wa Barcelona ni kwamba kiungo Sergio Busquets amesaini Mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo katika siku ya kusherehekea kuzaliwa kwake, na atakuwa mali ya Nou Camp hadi Juni 2018.
    Mkataba huo ambao una nafasi ya kurefushwa hadi mwaka 2019, wakati mshahara wa mchezaji huyo unabaki Pauni Milioni 130.
    Busquets, anayetimiza miaka 25 leo, ni shujaa wa Barcelona na ameichezea timu hiyo mechi 238.
    Staying power: Busquets has extended his deal at Barca by a further four years
    Bado wa nguvu: Busquets ameongeza Mkataba wa miaka minne Barca
    Barca boys: The Catalan giants have begun their pre-season training
    Vijana wa Barca: Vigogo wa Katalunya wameanza mazoezi ya kujiandaa na msimu
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: PIGO TENA MAN UNITED, FABREGAS AWATOLEA MBAVUNI TENA ILE KINOMA NOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top