• HABARI MPYA

    Wednesday, July 17, 2013

    CHELSEA: NDIYO, TUMEPELEKA OFA MAN UNITED KWA AJILI YA ROONEY, LAKINI HATUTOI MCHEZAJI WETU YEYOTE

    IMEWEKWA JULAI 17, 2013 SAA 9:50 ALASIRI
    KLABU ya Chelsea imethibitisha wameandika barua rasmi ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Wayne Rooney anayetaka kuondoka, lakini Manchester United imekataa ofa yao ya awali.
    BIN ZUBEIRY iliripoti mapema leo kwamba ofa hiyo ni David Luiz au Juan Mata pamoja na Pauni Milioni 10, lakini Chelsea imekanusha wachezaji hao wawili kuwapo katika dili hilo.
    Taarifa ya Chelsea imesomeka: "Chelsea FC inathibitisha kwamba jana waliandika barua rasmi ya ofa kwa Manchester United kwa ajili ya uhamisho wa Wayne Rooney,".
    Manchester United imekataa ofa hiyo ya kwanza ya Chelsea kwa ajili ya Wayne Rooney.
    United imesema Rooney hauzwi na kocha wa Chelsea, Jose Mourinho sasa lazima aamue kuweka fungu tu la maana la fedha mezani.
    Something on your mind? Wayne Rooney arrives at Manchester United's training ground on Wednesday
    Lolote mawazoni mwako? Wayne Rooney akiwasili viwanja vya mazoezi vya Manchester United leo kwa mazoezi

    Arsenal pia imetoa ofa ya awali ingawa pia imetoa ofa kwa Luis Suarez na Gonzalo Higuain.Klabu hiyo ya Stamford Bridge imeonywa, isithubutu kurejea na ofa ya pili, kwani United haina mpango wa kumuuza Rooney kwa klabu nyingine ya Ligi Kuu England.
    Inaonekana Mourinho yu tayari kuwauza Mata na Luiz, ili fedha atakazopata kutokana na mauzo ya wawili hayo atumie kumnunua mchezaji wa United.
    Rooney anafikiri amefikia kilele cha mustakabali wake na hana zaidi cha kuthibitisha baada ya misimu tisa Old Trafford. Inafahamika mshambuliaji huyo wa England amechanganyikiwa na kukerwa na maneno ya kocha mpya, David Moyes kwamba hatauzwa sababu ndiye mbadala wa mshambuliaji chaguo la kwanza, Robin van Persie.
    Mourinho aliwasha moto jana katika jitihada zake za kuwania saini ya Rooney kwa kutoa onyo kwamba, matumaini ya England yatakuwa madogo Kombe la Dunia kama mchezaji huyo atabakia United. 
    Chelsea imehamishia nguvu zake kwa Rooney baada ya wachezaji iliyokuwa inawataka awali kuwakosa wote, Radamel Falcao amekwenda Monaco na Edinson Cavani katua PSG, zote za Ufaransa.
    Mourinho alisema: "Ikiwa Wayne ni chaguo la pili kwa Manchester United, kisha timu ya taifa itaathirika.’
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: CHELSEA: NDIYO, TUMEPELEKA OFA MAN UNITED KWA AJILI YA ROONEY, LAKINI HATUTOI MCHEZAJI WETU YEYOTE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top