• HABARI MPYA

  Thursday, April 04, 2024

  TABORA UNITED YAICHAPA FOUNTAIN GATE 3-0 NA KUTINGA ROBO FAINALI KOMBE LA TFF


  TIMU ya Tabora United imefanikiwa kutinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Singida Fountain Gate leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  Mabao ya Tabora United leo yamefungwa na Najim Mussa dakika ya 48 na Patrick Lembo mawili dakika ya 71 na 90+4.
  Inakuwa timu ya tatu kutinga Robo Fainali baada ya Geita Gold iliyoitoa Rhino Rangers ya Tabora kwa kuichapa 2-1 jana Uwanja wa shule ya sekondari ya wasichana ya Nyankumbu mjini Geita na Namungo FC iliyoitoa Kagera Sugar kwa penalti 5-3 kufuatia sare ya bila kufungana juzi Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TABORA UNITED YAICHAPA FOUNTAIN GATE 3-0 NA KUTINGA ROBO FAINALI KOMBE LA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top