• HABARI MPYA

  Thursday, April 04, 2024

  BENCHIKA: HATUKUJA MISRI KUFUNGWA, TUMEJIPANGA KUWAKABILI AL AHLY


  KOCHA Mualgeria wa Simba SC, Abdelhak Benchika amesema kwamba mchezo wa kesho dhidi ya wenyeji, Al Ahly Jijini Cairo utakuwa mgumu, lakini wamejipanga kuwakabili mabingwa wa Afrika.
  Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari leo Jijini Cairo, Benchika amesema kwamba hawapo Misri kwa ajili ya kufungwa, bali kushindana na hawahofii chochote.
  "Hatujaja kufungwa hapa Misri, kama tungejua tunakuja kufungwa tusingekuja kabisa. Tumekuja kushindana, wala hatuhofii chochote. Itakuwa mechi ngumu, lakini tumejipanga kuwakabili,"amesema Benchika.
  Kwa upande wake, beki Mcameroon aliyeyewakililisha wachezaji wenzake wa Simba SC, Che Fondoh Malone Junior amesema kwamba wamejipanga vizuri na hawatahofia kelele za mashabiki wengi wa Al Ahly. 
  "Kuna tofauti ya kucheza nyumbani na ugenini, lakini mpira ni ule ule, mashabiki wao hawawezi kutuathiri chochote. Sisi tutajikita na yale yanayotokea uwanjani tu,"amesema Malone Junior. 
  Simba kesho watakuwa wageni wa Al Ahly katika mchezo wa marudiano Robó Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kuanzia Saa 5:00 usiku Uwanja wa Cairo international Jijini Cairo.
  Simba wanakabiliwa na shinikizo la kushinda ugenini kufuatia kufungwa 1-0 na mabingwa hao watetezi kwenye mechi ya kwanza Ijumaa iliyopita Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mshindi wa jumla katí ya Al Ahly na Simba atakwenda kumenyana na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Petro de Luanda ya Angola katika Nusu Fainali, ambazo mechi ya kwanza zilitoka sare ya 0-0 Jijini Lubumbashi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BENCHIKA: HATUKUJA MISRI KUFUNGWA, TUMEJIPANGA KUWAKABILI AL AHLY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top