• HABARI MPYA

    Thursday, June 01, 2023

    SIMBA WALIVYOREJEA DAR BAADA YA KUIPIGA MUFURILA 5-0 ZAMBIA 1979

     


    WACHEZAJI wa Simba SC kuanzia chini kwenda juu, kipa Athumani Mambosasa (sasa marehemu), George ‘Best’ Kulagwa, Abbas Kuka, Saad Ally, Hussein Tindwa (sasa marehemu) na Hamisi Askari (marehemu pia) wakiteremka kwenye ndege baada ya kuwasili kutoka Zambia ambako waliwafunga wenyeji, Mufulira Wanderers 5-0 katika mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1979. 
    Simba SC ikafuzu kwa ushindi wa jumla wa 5-4 kufuatia kufungwa 4-0 na Mufurila Wanderers Dar es Salaam. Safari ya Simba iliishia raundi ya Pili ambako ilitolewa na Raccah Rovers, ikitoa sare ya 0-0 Dar es Salaam kabla ya kwenda kufungwa 2-0 Nigeria.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA WALIVYOREJEA DAR BAADA YA KUIPIGA MUFURILA 5-0 ZAMBIA 1979 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top