• HABARI MPYA

  Thursday, June 01, 2023

  SEVILLA WABEBA EUROPA LEAGUE KWA MARA YA SABA


  TIMU ya Sevilla ya Hispania imefanikiwa kutwaa Kombe la Europa League kwa mara ya saba baada ya ushindi wa penalti 4-1 kufuatia sare ya 1-1 na AS Roma usiku wa Jumatano Uwanja wa Puskás Aréna Jijini Budapest nchini Hungary.
  Roma ya kocha José Mourinho ilitangulia kwa bao la dakika ya 34 la Paulo Dybala, kabla ya Gianluca Mancini kujifunga dakika ya 55 kuipatia bao la kusawazisha Sevilla.
  Na kwenye mikwaju ya penalti Bryan Cristante pekee alifunga ya Roma, huku za Sevilla zikifungwa na Lucas Ocampos, Erik Lamela, Ivan Rakitić na Gonzalo Montiel.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SEVILLA WABEBA EUROPA LEAGUE KWA MARA YA SABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top