• HABARI MPYA

  Friday, March 11, 2022

  WAZIRI WA ZANZIBAR MGENI RASMI SIMBA NA GENDARMERIE


  WAZIRI wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Zanzibar, Omar Said Shaaban atakuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika baina ya wenyeji, Simba SC dhidi ya RS Berkane ya Morocco.
  Mchezo huo wa Kundi D utafanyika Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam na kurushwa moja kwa moja na chaneli ya UTV ya Azam Tv kuanzia Saa 10:00 jioni.
  Mechi ya kwanza wiki iliyopita Berkane ilishinda 2-0 mjini Berkane na sasa ndio inaongoza Kundi hilo kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na Simba na US Gendamarie ya Niger zenye pointi nne kila moja, wakati ASEC ya Ivory Cost yenye pointi tatu inashika mkia baada ya mechi tatu za awali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAZIRI WA ZANZIBAR MGENI RASMI SIMBA NA GENDARMERIE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top