• HABARI MPYA

  Sunday, March 06, 2022

  MANCHESTER CITY YAIFUMUA UNITED 4-1 ETIHAD


  WENYEJI, Manchester City wamewafumua jirani zao, Manchester United mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Mabao ya Man City yamefungwa na Kevin De Bruyne mawili dakika ya tano na 28 na Riyad Mahrez mawili pia, dakika ya 68 na 90, wakati la Man United limefungwa na Jadon Sancho dakika ya 22.
  Kwa ushindi huo mnono, timu ya kocha Mspaniola, Pep Guardiola inafikisha pointi 69 katika mchezo wa 28 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi sita zaidi ya Liverpool wanaofuatia, ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi.
  Kipigo cha leo kinazidi kupunguza matumaini ya Man United iliyo chini ya kocha wa muda, Mjerumani, Ralf Rangnick kumaliza nafasi nne za juu, ili ikibaki na pointi zake 47 za mechi 28 nafasi ya tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANCHESTER CITY YAIFUMUA UNITED 4-1 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top