• HABARI MPYA

  Monday, March 21, 2022

  MAN CITY YAIFUATA LIVERPOOL KIBABE WEMBLEY


  TIMU ya Manchester City imetinga Nusu Fainali ya Kombe la FA England kwa kishindo baada ya kuwachapa wenyeji,Southampton mabao 4-1 Jumapili Uwanja wa St. Mary's mjini Southampton, Hampshire.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na Raheem Sterling dakika ya 12, Kevin De Bruyne dakika ya 62 kwa penalti, Phil Foden dakika ya 75 na Riyad Mahrez dakika ya 78, wakati la Southampton limefungwa na Aymeric Laporte aliyejifunga dakika ya 45 na ushei.
  Sasa Man City itakutana na wapinzani wao katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England, Liverpool mwezi ujao Uwanja wa Wembley Jijini London.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAIFUATA LIVERPOOL KIBABE WEMBLEY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top