// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); RAIS SAMIA AWACHANGIA SH MILIONI 15 TWIGA STARS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE RAIS SAMIA AWACHANGIA SH MILIONI 15 TWIGA STARS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Wednesday, March 09, 2022

  RAIS SAMIA AWACHANGIA SH MILIONI 15 TWIGA STARS


  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan ameahidi kuichangia timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars kiasi Sh. Milioni 15. 
  Rais Samia alitoa ahadi hiyo wakati akizungumza kwa simu na Waziri wa Fedha na Mipango,  Mwigulu Nchemba kwenye tamasha la harambee ya kuchangia Twiga Stars lililopewa jina, Orange Concect.
  Kwa upande wake, Waziri Nchemba ametoa wito kwa makampuni mbalimbali kutoa udhamini kwenye timu za wanawake ili ziweze kuendelea kufanya vizuri.
  Nchemba amesema Mheshimiwa Rais amefanya mambo makubwa siyo tu kwenye sekta ya Michezo bali katika sekta mbalimbali.


  Ametaja baadhi ya mambo makubwa ambayo Serikali imefanya kuwa ni maboresho makubwa kwenye huduma za jamii.
  Pia amesema Mhe. Rais alivyoingia madarakani alielekeza watoa huduma walipwe madeni na maisha yao yameboreka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS SAMIA AWACHANGIA SH MILIONI 15 TWIGA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top