• HABARI MPYA

    Sunday, March 13, 2022

    RONALDO AVUNJA REKODI YA MABAO YA FIFA


    MSHAMBULIAJI Mreno, Cristiano Ronaldo jana amevunja rekodi ya mabao ya FIFA baada ya kufunga hat-trick akiiwezesha Manchester United kushinda 3-1 dhidi ya Tottenham Hotspur kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford. 
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 sasa amefikisha mabao 807, akimpiku Josef Bican, aliyekuwa anashikilia rekodi hiyo.
    Ronaldo alifunga mabao yake dakika za 12, 38 na 81, wakati mabao ya Spurs yalifungwa na Harry Kane kwa penalti dakika ya 35 na Harry Maguire aliyejifunga dakika ya 72.
    Ushindi huo unaifanya Man United ifikishe pointi 50 katika mchezo wa 29 na kurejea nafasi ya nne, ikiizidi pointi mbili Arsenal, ambayo hata hivyo ina mechi nne mkononi, wakati Spurs inabaki na pointi zake 45 za mechi 27 sasa nafasi ya saba.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RONALDO AVUNJA REKODI YA MABAO YA FIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top