• HABARI MPYA

  Sunday, March 06, 2022

  ARSENAL YAICHAPA WATFORD 3-2 VICARAGE


  TIMU ya Arsenal imeibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya wenyeji, Watford katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Vicarage Road mjini Watford.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Martin Odegaard dakika ya tano, Bukayo Saka dakika ya 30 na Gabriel Martinelli dakika ya 52, wakati ya Watford yamefungwa na Cucho Hernandez dakika ya 11 na Moussa Sissoko dakika ya 87.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 48 katika mchezo wa 25 na kupanda nafasi ya nne, wakati Watford inabaki na pointi zake 19 za mechi 27, nafasi ya 19.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAICHAPA WATFORD 3-2 VICARAGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top