• HABARI MPYA

  Saturday, March 05, 2022

  AZAM FC YACHAPWA 1-0 NA POLISI CHAMAZI


  WENYEJI, Azam FC wamechapwa 1-0 na Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Bao pekee la Polisi Tanzania limefungwa na mshambuliaji Shaaban Kassim Haruna dakika ya 41 na kwa ushindi huo, Maafande hao wanafikisha pointi 22 katika mchezo wa 17, wakati Azam FC inabaki  na pointi zake 25 za mechi 17 pia nafasi y tatu.
  Katika mchezo uliotangulia, Mbeya Kwanza ililazimishwa sare ya bila mabao na Mbeya City Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma.
  Mbeya Kwanza inafikisha pointi 14 katika mechi ya 17 nafasi ya 15 na Mbeya City inatimiza pointi 25 mechi 17 pia nafasi ya tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YACHAPWA 1-0 NA POLISI CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top