• HABARI MPYA

  Saturday, March 19, 2022

  YANGA YAIPASUA KMC 2-0 MBELE YA MZEE KIKWETE


  VIGOGO, Yanga wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa KMC mabao 2-0 usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Katika mchezo huo uliohudhuriwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete, bao la kwanza la Yanga beki wa zamani wa timu hiyo, Andrew Vincent ‘Dante’ alijifunga dakika ya 39 katika harakati za kuokoa mpira uliounganishwa na mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele.
  Na bao la pili akafunga beki Mkongo, Djuma Shaaban dakika ya 52, akiwa ametoka kutia krosi iliyosab

  abisha bao la kwanza.
  Kwa ushindi huo, Yanga wanafikisha pointi 48 katika mchezo wa 18 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi 11 zaidi ya  mabingwa watetezi, Simba ambao pia wana mechi moja mkononi.
  KMC baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake 22 za mechi 18, nafasi ya saba.
  Mechi hiyo ilikwenda sambamba na sherehe za kuzimisha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani na viongozi wa Yanga walicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Wasanii na kuibuka na ushindi wa 2-1.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAIPASUA KMC 2-0 MBELE YA MZEE KIKWETE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top