• HABARI MPYA

  Sunday, March 27, 2022

  KIDUKU ATWAA UBINGWA WA AFRIKA


  BONDIA Mtanzania, Twaha Kassim Rubaha ‘Twaha Kiduku’ jana amefanikiwa kutwaa taji la ubingwa wa Afrika wa UBO uzito wa Super Middle baada ya ushindi wa pointi dhidi ya Mkongo Alexandre Kabangu Tshiamuandaukumbi wa Tanzanite Hall mjini Morogoro.
  Kiduku anafikisha mapambano 19 ya kushinda, akiwa amepoteza, moja droo na manane ya kupigwa, saba akiwa amepigwa nje ya nchi – moja tu alichapwa na mwamba anaitwa Idd Pialari Desemba 25, mwaka 2016 PTA Saba Saba, Dar es Salaam, ambalo lilikuwa pambano lake la tisa la ngumi za kulipwa.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIDUKU ATWAA UBINGWA WA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top