• HABARI MPYA

  Saturday, March 05, 2022

  CHELSEA YAISHINDILIA BURNLEY 4-0 TURF MOOR


  WENYEJI, Burnley wametandikwa mabao 4-0 na Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Turf Moor.
  Mabao ya timu ya kocha Mjerumani, Thomas Tuchel yamefungwa na Reece James dakika ya 47, Kai Havertz mawili dakika ya 52 na 55 na Christian Pulisic dakika ya 69.
  Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 53, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi saba na Liverpool baada ya timu zote kucheza mechi 26, wakati Burnley inabaki na pointi zake 21 za mechi 26 nafasi ya 18.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAISHINDILIA BURNLEY 4-0 TURF MOOR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top