• HABARI MPYA

  Sunday, March 13, 2022

  SIMBA YAICHAPA BERKANE 1-0 NA KUONGOZA KUNDI


  BAO la Pape Ousmane Sakho dakika ya 44 limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya RS Berkane ya Morocco katika mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. 
  Winga huyo Msenegal alifunga bao hilo akimalizia pasi ya Mnyarwanda, Meddie Kagere na kwa ushindi huo, Simba inafikisha pointi saba na kupanda kileleni mwa kundi hilo, ikiizidi pointi moja Berkane. 
  Mechi nyingine ya Kundi hilo inafuatia Saa 1:00 usiku huu mjini Cotonou nchini Benin baina ya ASEC MIMOSAS ya Ivory Coast na US Gendamarie ya Niger kukamilisha mzunguko wa nne.
  Kwa sasa Gendamarie ina pointi nne na ASEC pointi tatu baada ya mechi tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAICHAPA BERKANE 1-0 NA KUONGOZA KUNDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top