• HABARI MPYA

  Tuesday, March 22, 2022

  ADI AONGEZWA KIKOSINI TAIFA STARS


  MSHAMBULIAJI wa Yeovil Town ya England, Adi Yussuf ameongezwa kwenye kikosi cha ya taifa ya Tanzania kwa ajili ya mechi tatu za kirafiki kwenye kalenda ya FIFA
  Taifa Stars kesho inashuka dimbani Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kumenyana na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) katika mchezo wa kirafiki.
  Stars iliyo chini ya kocha Mdenmark, Kim Poulsen itakuwa na mechi tatu jumla, nyingine dhidi ya Botawana Machi 26 na dhidi ya Sudan Machi 29, mechi zote zikipigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
  CAR na Sudan zitamenyana pia baina yao Machi 26.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ADI AONGEZWA KIKOSINI TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top