• HABARI MPYA

  Saturday, March 12, 2022

  YANGA NA SOMALIA 1-1 MECHI YA HISANI CHAMAZI


  VIGOGO, Yanga SC wamelazimishwa sare ya 1-1 na timu ya taifa ya Somalia katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Azam Comolex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Zakaria alianza kuifungia Somalia dakika ya 18, kabla ya Mkongo Chico Ushindi kuisawazishia Yanga dakika sita baadaye.
  Huo ulikuwa mchezo maalum kuchangia taasisi ya Ally Kimara Foundation, kijana anayesumbuliwa na maradhi adimu aliyeanzisha mfuko huo kusaidia watoto wengine wote wnaosumbuliwa na maradhi hayo.


  Mapema kabla ya mchezo huo,  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan alipiga simu na kuahidi kuchangia Sh. Milioni 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA NA SOMALIA 1-1 MECHI YA HISANI CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top