• HABARI MPYA

  Sunday, March 20, 2022

  TANZANIA YASONGA MBELE KOMBE LA DUNIA WASICHANA U17


  TIMU  ya taifa ya wasichana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, leo imefanikiwa kwenda Raundi ya Tatu kufuzu Kombe la Dunia baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya wenyeji, Botswana leo Uwanja wa Francistown mjini Francistown.
  Mabao ya Tanzania yamefungwa na Neema Kinega dakika ya 28 na Clara Luvanga matatu dakika za 62, 63 na 81 na kwa matokeo hayo inafuzu kwa ushindi wa jumla wa 11-0 kufuatia kuwachapa Botswana 8-0 kwenye mechi ya kwanza Zanzibar.
  Sasa Tanzania itamenyana na Burundi kuwania kuingia hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya India baadaye mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA YASONGA MBELE KOMBE LA DUNIA WASICHANA U17 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top