• HABARI MPYA

  Thursday, March 03, 2022

  CANELO ALVAREZ NA DMITRY BIVOL KUZIPIGA MEI 7


  MABONDIA Saul 'Canelo' Alvarez na Dmitry Bivol watapanda ulingoni Mei 7 ukumbi wa T-Mobile Arena, Jijini Las Vegas, Marekani kuwania ubingwa wa dunia wa WBA uzito wa Light Heavy.
  Katika usiku huo, mabondia kutoka Urusi na Belarus wataruhusiwa kupigana, lakini bila bendera zao kupeperushwa au kuchezwa wimbo wao mataifa yao – na tayari WBA imewaondoa kwenye rankings zake mabondia wote wan chi hizo.
  Bivol ni mzaliwa Kyrgyzstan, wazazi wake wanatoka Moldova na Korea, lakini anaishi Urusi, ambaye alitwaa taji hilo la WBA Light Heavy mwaka 2016 na amekwishalitetea mara 10 tayari.
  Mmexico, Canelo ni bingwa wa kwanza asiyepingika wa uzito wa Super-Middle ambaye ameongeza mataji ya IBF, WBA (Super), WBC, WBO baada ya kumpiga Mmarekani, Caleb Plant mwezi Novemba ambaye amempandia uzito Bivol.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CANELO ALVAREZ NA DMITRY BIVOL KUZIPIGA MEI 7 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top