• HABARI MPYA

  Friday, March 04, 2022

  M-BET YAWAZAWADIA WASHINDI PERFECT 12 SH MILIONI 226.5

  KAMPUNI ya mchezo ya kubahatisha ya M-BET Tanzania imezidi kumwaga fedha baada ya kumzawadia shabiki wa timu ya Yanga na Chelsea Peter Nangi kitita cha Sh milioni 50.

  Nangi ambaye ni mkazi wa Geita, ameshinda kiasi hicho cha fedha  baada ya kubashiri kwa usahihi jumla ya michezo 12 ya mchezo wa kubahatisha wa Perfect12wa kampuni ya M-Bet Tanzania.

  Mkurugenzi Masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa Nangi ameibuka mshindi ikiwa siku moja tu baada ya Shabiki wa klabu ya Simba na Arsenal Swalehe Enzi ameshinda kitita cha sh 176,470,910 kupitia pia Perfect12 wa kampuni ya M-Bet Tanzania.


  Shabiki wa Yanga na timu ya Chelsea, Peter Nangiakipozi baada ya kuzawadiwa mfano wa hundi baada yakufanikiwa kubashiriki kwa usahihi mechi 12 za  ligimbalimbali dunianiNangi alizawadiwa Sh50 milioni


  “ M-Bet sasa imeanzisha kampeni mpya inayoitwaZALI LA M-BET ambapo ukicheza na M-Bet unawezajishindia Pikipiki na pesa taslimu kila wiki hukuMwishio wa kampeni mshindi mmoja ataondoka naToyota IST,” Mushi.

  Kwa upande wake, Nangi alisema kuwa ushindi wake umetokana na kuwa makini katika kuchagua timu bila ya kufauata alama za ushindi ambazo kila timu imekuwa ikipewa katika mkeka.

  Alisema kuwa alianza kubet miezi sita iliyopita naushindi huu umempa faraja kubwa sana kwani ataongeza mtaji wake na kujishughulisha zaidi na kilimo.

  “Siri kubwa ya kushinda bahati nasibu hii kujua uwezo wa timu pamoja na kufanyia utafiti wa timu, aina ya wachezaji ambao wamesajili, aina ya timu unayocheza nayo pamoja na majeruhi.

  Ukibet kwa kupenda timu yako, unapotea kwani lazima uwe mfuatiliaji wa michezo mbalimbali. Kama unajua inafungwa, tabiri hivyo na weka mapenzi pembeni kwenye shughuli hii,” alisema Nangi.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: M-BET YAWAZAWADIA WASHINDI PERFECT 12 SH MILIONI 226.5 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top