• HABARI MPYA

  Saturday, March 19, 2022

  AZAM FC YAWACHAPA WASOMALI 3-1 CHAMAZI


  WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 ya Somalia katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 64, Idris Mbombo dakika ya 81 na Shaaban Iddi Chilunda dakika ya 90 na ushei.
  Somalia U23 katika mchezo wao wa kwanza wa kirafiki walitoka sare ya 1-1 na vigogo, Yanga hapo hapo Azam Complex.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAWACHAPA WASOMALI 3-1 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top