• HABARI MPYA

  Thursday, March 17, 2022

  PUMZIKA KWA AMANI JOHN POMBE MAGUFULI


  MACHI 8 mwaka 2020, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DK John Pombe Joseph Magufuli alikuwa mgeni rasmi katika pambano la watani wa jadi, Yanga ikifuta uteja uliodumu kwa miaka minne mbele ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC baada ya ushindi wa 1-0 jioni ya leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
  Shujaa wa Yanga SC ni leo kiungo mshambuliaji Mghana, Bernard Morrison aliyefunga bao hilo pekee la ushindi dakika ya 44 kwa shuti la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 25.
  Morrison, mchezaji wa zamani wa Heart of Lions, Ashanti Gold za kwao Ghana, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Delhi Dynamos FC ya India na Orlando Pirates ya Afrika Kusini alifunga bao hilo baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na kungo Jonas Gerlad Mkude. 
  Baada ya msimu huo, Morrison akahamia kwa watani wa jadi, Yanga.
  Machi 26, mwaka 2021 Magufuli akafariki dunia na leo Watanzania wanaazimisha mwaka mmoja tangu kifo cha mpendwa wao huyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PUMZIKA KWA AMANI JOHN POMBE MAGUFULI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top