• HABARI MPYA

  Sunday, March 27, 2022

  DTB YAENDELEZA UBABE CHAMPIONSHIP

  TIMU ya DTB imeendeleza ubabe katika mbio za kuwania kupanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara kupitia michuano ya Championship baada ya ushindi wa 2-1 jana dhidi ya Transit Camp Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
  Mabao ya DTB yalifungwa na Johnson Clement na Mghana Nicholas Gyan  la Transit Camp lilifungwa na Kalegea Wazanga.
  Katika mchezo huo, timu zote zilimaliza, DTB wakimpoteza mshambuliaji wao Mrundi, Amissi Tambwe na Transit wakiwapoteza Wazanga na Omar Shaaban waliotolewa kwa kadi nyekundu.
  Kwa matokeo hayo, DTB inafikisha pointi 52 na kuendelea kuongoza Championship kwa pointi tano zaidi ya zote, Ihefu SC ya Mbeya na Kitayosce ya Tabora baada ya timu zote kucheza mechi 22.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DTB YAENDELEZA UBABE CHAMPIONSHIP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top