• HABARI MPYA

  Wednesday, March 16, 2022

  AZAM FC YAICHAPA NAMUNGO 2-1 RUANGWA


  TIMU ya Azam FC imezinduka na kupata ushindi wa ugenini wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Namungo FC jioni ya leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na Prince Dube Mpumelelo dakika ya 22 na Ismail Aziz Kader dakika ya 35, baada ya Namungo FC kutangulia na bao l Mohammed Issa dakika ya pili.
  Azam FC inafikisha pointi 28 baada ya ushindi huo na kurejea nafasi ya tatu, ikiizidi pointi tatu Namungo baada ya wote kucheza mechi 18.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA NAMUNGO 2-1 RUANGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top