• HABARI MPYA

    Tuesday, March 08, 2022

    SPORTPESA YAZINDUA KAMPENI YA KUWAZAWADIA WATEJA WAKE

    KAMPUNI ya michezo na burudani SportPesa imezindua rasmi kampeni maalumu kwa ajili ya kuwazawadia wateja wake.
    Promosheni hii imezinduliwa leo katika ofisi zao Masaki, Dar es Salaam ikihusisha makampuni ya mitandao ya simu Vodacom na Airtel ikiwa na lengo la kuwazawadia wateja hasa katika kipindi hiki ambapo mechi mbalimbali zinaendelea.
    Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Sportpesa Tarimba Abbas alisema katika kipindi hiki tumeona tuwazawadie wateja wetu wote kwa kuzindua promosheni inayoenda kwa jina la “Bet Bonanza”.


    Promosheni hii inaanza rasmi leo na na itadumu kwa muda wa siku 35. Kutakuwa na washindi wa kila siku ambao watajishindia kiasi cha shilingi elfu 20 kila mmoja, kila siku, na washindi wa shilingi milioni moja moja kila wiki na mwisho wa promosheni tutatoa 15,888,000/- kwa mshindi mwenye bahati”.
    “Droo zitachezwa kila siku na washindi watatangazwa kupitia kurasa za mitandao ya kijamii zetu na za washirika wetu Vodacom, na Airtel, pamoja na kurasa za timu tunazozidhamini Simba,Yanga na Namungo”
    “Ili kushiriki kwenye promosheni hii ni lazima kuweka pesa kuwenye akaunti yako ya SportPesa na kuanza kucheza ili kuingia kwenye droo ili kupata nafasi ya kuibuka mshindi, kwa wateja wapya watatakiwa kujisajili kwanza kisha kufuata mtirirko huo huo”.
    “Napenda kuwakaribisha watumiaji wa mitandao yote kushiriki kwenye promosheni hii hata wale ambao hawajajisajili na SportPesa ili waweze kushinda zawadi za kila siku, kila wiki na zawadi kubwa kabisa ya zaidi ya shilingi milioni 15” alimaliza Tarimba.
    Kwa upande wake Meneja Mauzo wa M-Pesa, kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania PLC Kelvin Nyanda alisema, tumeamus kushirikiana na Sportpesa kwa sababu kuna ligi mbali mbali zinazoendelea kama Champions league, NBC Premier League, English premier league, league 1 etc ambazo zitawapa fursa wateja wetu kwa siku 35 kujinyakulia kiasi cha shilingi elfu 20 kila siku, milioni moja moja kwa wiki na zawadi kubwa ya zaidi ya milioni 15, mwisho wa kampeni. Na hivyo kupata washindi wa mwezi mzima.
    Kushiriki ni rahisi sana, kila mteja wa M-Pesa ana nafasi ya kushinda katika kipindi hiki kwa kuingia kwenye menyu ya malipo ya M-Pesa kisha chagua lipa bili, halafu michezo, kisha SportPesa, halafu fuata maelezo.
    Ukimaliza utapata majibu papo hapo kuwa umeingia kwenye droo ya siku/wiki/mwezi, na washindi watapigiwa simu kujulishwa kuwa wameshinda na majina yatatangazwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii (Social media pages) za SportPesa.
    “Napenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisha wateja wetu kushiriki mara nyingi wawezavyo, maana ushindi upo kwa ajili yao.
    Akizungumza kutoka Airtel Meneja mauzo, biashara MPesa Aggrey Charles alisema,
    “Katika msimu huu kuna mechi mbalimbali zinaendelea tumeona ni vizuri kushirikiana na washirika wetu SportPesa ili wateja wetu wa Airtel ili waweze kubashiri kwa urahisi na kupata nafasi ya kujishindia mamilioni ya pesa”
    Kushiriki ni rahisi, mteja wa Airtel anapaswa kujisajili na Sportpesa na kuweka pesa kwenye akauti yake ya SportPesa kupitia huduma ya Airtel Money kubashiri mechi anayoipenda na kupata nafasi ya kuingia kwenye droo ili kujishindia zawadi za kila siku, wiki na hatimae zawadi ya mwisho wa promosheni ambayo ni shilingi 15,888,000/-.”
    “Kumbuka mteja wa Airtel kupitia huduma ya Airtel Money anaweza kuweka pesa kwenye akaunti ya SportPesa kwa kupiga *150*60# au kupitia Airtel Money App au kupitia www.sportpesa.co.tz
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SPORTPESA YAZINDUA KAMPENI YA KUWAZAWADIA WATEJA WAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top