• HABARI MPYA

  Thursday, March 03, 2022

  ABRAMOVICH AIWEKA SOKONI CHELSEA DOLA BILIONI 3


  VYOMBO vya habari Uingereza vimeripoti kwamba bilionea Mrusi, Roman Abramovich mmiliki wa Chelsea anaiuza klabu hiyo.
  Bilionea wa Kiswiss, Hansjorg Wyss yupo kwenye nafasi nzuri ya kuinunua dhidi ya mabilionea wa Marekani kwa dau la dola za Kimarekani Bilioni 3.
  Roman Abramovich anatafuta mnunuzi wa haraka wa klabu hiyo baada ya kuwekewa vikwazo vingi kufuatia majeshi yanchi yake, Urusi kuvamia na kuishambulia Ukraine kwa wiki ya pili sasa.
  Taarifa zaidi zinasema Bilione huyo aliyeanza kuimiliki mwaka 2003 anauza pia na majengo na mali zake nyingine Uingereza kuepuka kutaifishwa.
  Abramovich ameweza zaidi ya dola Bilioni 2 tangu ainunue Chelsea na kuifanya kuwa moja ya klabu kubwa Ulaya na yenye mafanikio zaidi England ikitwaa mataji 19 chini yake na ndio mabingwa wa sasa wa Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ABRAMOVICH AIWEKA SOKONI CHELSEA DOLA BILIONI 3 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top