• HABARI MPYA

  Sunday, March 06, 2022

  MABINTI WA TANZANIA WAWACHAPA BOTSWANA 7-0


  TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17, imeitandika Botswana mabao 7-0 jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar katika mchezo wa Raundi ya Pili kufuzu Kombe la Dunia baadaye mwaka huu nchini India.
  Mabao ya Tanzania U17 leo yamefungwa na Neema Paul na Clara Luvanga kila mmoja mawili na Aisha Juma matatu.
  Timu hizo zitarudiana Machi 20 Uwanja wa Obed Itani Chilume  Jijini Francistown na mshindi wa jumla atakutana na Burundi katika Raundi ya Tatu kuwania kwenda Raundi ya mwisho ya mchujo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MABINTI WA TANZANIA WAWACHAPA BOTSWANA 7-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top