• HABARI MPYA

  Thursday, March 03, 2022

  SONG KOCHA MKUU MPYA CAMEROON


  BEKI wa zamani wa Liverpool na West Ham United, Rigobert Song (45) amethibitishwa kuwa kocha mpya Mkuu wa Cameroon kwa agizo la Rais wan chi hiyo, Paul Biya nyota huyo wa zamani wa Simba Wasiofungika, akichukua nafasi ya Toni Conceicao, aliyeshindwa kuipa timu taji la AFCON nyumbani mwezi uliopita, ikimaliza nafasi ya tatu.
  Song ndiye mchezaji aliyeichezea mechi nyingi aidi Cameroon, 137 na amewahi kuwa kocha muda wa timu hiyo mwaka 2018.
  Conceicao amesaidia Cameroon kufika hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya Kombe la Dunia na watamenyana na Algeria katika mechi mbili za nyumbani na ugenini kuwania tiketi ya Qatar baadaye mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SONG KOCHA MKUU MPYA CAMEROON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top