• HABARI MPYA

  Sunday, March 13, 2022

  DODOMA JIJI YAICHAPA MBEYA KWANZA 2-0 JAMHURI

  WENYEJI, Dodoma Jiji FC wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbeya Kwanza katika mchezo wa Ligi ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Mabao ya Dodoma Jiji FC yamefungwa na Joram Mgeveke dakika ya 26 na Anuary Jabir dakika ya 48 na kwa ushindi huo, wanafikisha pointi 21 na kusogea nafasi ya 11, wakati Mbeya Kwanza wanabaki na pointi zao 14 katika nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 18.
  Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka moja kwa moja na mbili zitakwenda kucheza na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DODOMA JIJI YAICHAPA MBEYA KWANZA 2-0 JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top