• HABARI MPYA

  Monday, March 07, 2022

  SIMBA YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0, CHAMA NA KAGERE


  MABINGWA watetezi, Simba SC wameilaza Dodoma Jiji FC mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba yamefungwa na kiungo Mzambia, Clatous Chama dakika ya 56 kwa penalti na mshambuliaji Mnyarwanda, mzaliwa wa Uganda, Meddie Kagere dakika ya 74.
  Kwa ushindi huo, timu ya kocha Mspaniola, Pablo Franco Martin inafikisha pointi 37, ingawa inabaki  nafasi ya pili, ikizidiwa pointi nane na jirani zao, Yanga SC baada ya wote kucheza mechi 17.
  Katika mechi zilizotangulia leo, Ruvu Shooting imelazimishwa sare ya 0-0 na Biashara United Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, wakati Coastal Union imewachapa wenyeji, KMC 2-3 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Coastal Union yamefungwa na Abdul Hamisi kwa penalti dakika ya 22, William Kisingi dakika ya 82 na Rashid Chambo dakika ya 90 na ushei, wakati ya KMC yamefungwa na Emmanuel Mvuyekure dakika ya 40 na Kenny Ally dakika ya 47.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0, CHAMA NA KAGERE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top