• HABARI MPYA

  Sunday, March 20, 2022

  MANULA AOKOA PENALTI MBILI, SIMBA YAPIGWA 3-0


  MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamechapwa mabao 3-0 na wenyeji wahamiaji, ASEC Mimosas katika mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika leo Uwanja wa Jénérali Mathieu Kerekou​mjini Cotonou nchini Benin.
  Mabao ya ASEC yamefungwa na viungo Aubin Kramo Kouamé dakika ya 16, Mburkina Faso, Stephane Aziz Ki dakika ya 25 na mshambuliaji Karim Konaté dakika 57.
  Lakini sifa zimuendee kipa namba moja wa Tanzania, Aishi Salum Manula kwa kuokoa mikwaju miwili ya penalti ya Konaté dakika ya 36 na mshambuliaji mwingine, Anicet Alain Oura dakika ya 90.
  Kwa matokeo hayo, ASEC inafikisha pointi tisa na kupanda kileleni kwa Kundi D, ikizizidi pointi mbili Simba na RSB Berkane ya Morocco, wakati US Gendamarie inaendelea kushika mkia sasa ikifikisha pointi tano baada ya wote kucheza mechi tano kuelekea mechi za mwisho wikiendi ijayo.
  Wakati ASEC watamalizia ugenini dhidi ya Berkane, Simba watamalizia nyumbani na US Gendamarie kuwania nafasi mbili za juu ili kwenda Robo Fainali.
  Simba ndio inaongoza Kundi D kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na RSB Berkane pointi sita sawa na ASEC, wakati USGN inashika mkia kwa pointi zake tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANULA AOKOA PENALTI MBILI, SIMBA YAPIGWA 3-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top