• HABARI MPYA

  Thursday, March 10, 2022

  BENZEMA APIGA HAT TRICK REAL YAICHAPA PSG 3-1


  WENYEJI, Real Madrid wametinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Paris Saint-Germain usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Santiago Bernabéu Jijini Madrid, Hispania.
  Mabao yote ya Real Madrid yamefungwa na mshambuliaji mkongwe Mfaransa, Karim Benzema dakika za 61,76 na 78 baada ya PSG kutangulia kwa bao la mshambuliaji Mfaransa pia, Kylian Mbappe dakika ya 39.
  Real wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2, kufuatia kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wa 16 Bora Ufaransa, bao la Mbappe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BENZEMA APIGA HAT TRICK REAL YAICHAPA PSG 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top