• HABARI MPYA

  Sunday, March 13, 2022

  LIVEROOOL YAICHAPA BRIGHTON 2-0 UGENINI


  TIMU ya Liverpool jana imepata ushindi wa ugenini wa 2-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa The AMEX.
  Mabao ya Liverpool yalifungwa na Luis Diaz dakika ya 19 na Mohamed Salah kwa penalti dakika ya 61 baada ya Yves Bissouma kuunawa mpira.
  Kwa ushindi huo Liverpool inafikisha pointi 66, ingawa inabaki nafasi ya pili, ikizidiwa pointi tatu na Manchester City wanaoongoza, wakati Brighton inabaki na pointi zake 33 katika nafasi ya nane baada ya timu kucheza mechi 28.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVEROOOL YAICHAPA BRIGHTON 2-0 UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top