• HABARI MPYA

  Thursday, March 03, 2022

  FURY KUSTAAFU BAADA YA PAMBANO NA WHITE


  BINGWA wa dunia ngumi za kulipwa uzito wa juu, Tyson Fury amesema atastaafu baada ya pambano na Dillian Whyte Aprili 23, mwaka huu Uwanja wa Wembley Jijini London.
  Kauli hiyo inamaanisha ndoto za kushuhudia Gipsy King akizipiga na Muingereza mwenzake, Anthony Joshua au Oleksandr Usyk baadaye mwaka huu zinaweza zisitimie.
  Mbabe huyo mwenye umri wa miaka 33, Fury ambaye katika mapema ni yake 31 ametoa droo moja tu – hajapigana Uingereza tangu Agosti mwaka 2018 alipomchapa Francesco Pianeta mjini Belfast.
  Whyte, ambaye pia ana miaka 33, ameshinda mapambano 28 na kupigwa mawili kati ya 30 na ndiye mpinzani mkuu wa mkanda wa WBC uzito wa juu unaoshikiliwa na Fury.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FURY KUSTAAFU BAADA YA PAMBANO NA WHITE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top