• HABARI MPYA

  Wednesday, March 09, 2022

  LIVERPOOL YASINDIKIZWA ROBO FAINALI NA BAKORA


  WENYEJI, Liverpool wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kuchapwa 1-0 na Inter Milan ya Italia usiku wa jana Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool, England katika mchezo wa marudiano Hatua ya 16 Bora.
  Bao pekee la Inter jana lilifungwa na Lautaro Martinez dakika ya 61, kabla ya timu hiyo ya Milan kupata pigo kufuatia mshambuliaji wake, Alexis Sanchez kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 63 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.
  Liverpool inakwenda Robo Fainali kwa ushindi wa jumla wa 2-1 kufuatia kushinda 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Milan, mabao ya Roberto Firmino na Mo Salah.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YASINDIKIZWA ROBO FAINALI NA BAKORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top