• HABARI MPYA

  Saturday, March 05, 2022

  MANE AIFUNGIA BAO PEKEE LIVERPOOL YASHINDA 1-0


  BAO pekee la mshambuliaji Msenegal, Sadio Mane dakika ya 27, limeipa Liverpool ushindi wa 1-0 dhidi ya West Ham United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu Uwanja wa Anfield.
  Liverpool inafikisha pointi 63, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tatu tu na mabingwa watetezi, Manchester City baada ya kila timu kucheza mechi 27.
  West Ham United baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi 45 za mechi 28 nafasi ya tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANE AIFUNGIA BAO PEKEE LIVERPOOL YASHINDA 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top