• HABARI MPYA

  Monday, March 21, 2022

  AUBAMEYANG APIGA MBILI BARCA YAITANDIKA REAL 4-0


  TIMU ya Barcelona imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji, Real Madrid katika mchezo wa La Liga Jumapili Uwanja wa Santiago Bernabéu Jijini Madrid.
  Mabao ya Barcelona yamefungwa na Pierre-Emerick Aubameyang mawili, dakika ya 29 na 51, Ronald Araujo dakika ya 38 na Ferran Torres dakika ya 57.
  Kwa ushindi huo, Barcelona inafikisha pointi 54 katika mchezo wa 28 na kusogea nafasi ya tatu, sasa ikizidiwa pointi 12 na Real ambao pia wamecheza mechi moja zaidi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AUBAMEYANG APIGA MBILI BARCA YAITANDIKA REAL 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top