// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MAN UNITED YATUPWA NJE LIGI YA MABINGWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MAN UNITED YATUPWA NJE LIGI YA MABINGWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Wednesday, March 16, 2022

  MAN UNITED YATUPWA NJE LIGI YA MABINGWA


  WENYEJI, Manchester United wamechapwa 1-0 na Atlético Madrid, bao pekee la  Renan Lodi katika mchezo wa marudiano Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester, England.
  Kwa matokeo hayo, Atlético Madrid inakwenda Robo Fainali kwa ushindi wa jumla wa 2-1 baada ya sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Hispania.
  Nayo Benfica imewachapa wenyeji wengine, Ajax 1-0 bao pekee la Darwin  Núñez Ribeiro Uwanja wa Johan Cruijff Arena Jijini Amsterdam, Uholanzi hivyo kwenda Robo Fainali kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza Ureno.
  Timu nyingine zilizokwenda Robo Fainali ni Manchester City ya England iliyoitoa Sporting Lisbon ya Ureno, Real Madrid ya Hispania iliyoitoa PSG ya Ufaransa, Bayern Munich ya Ujerumani iliyoitoa Salzburg ya Austria, Liverpool ya England iliyoitoa Inter Milan ya Italia.
  Mechi za mwisho zinachezwa leo, Chelsea walioshinda 2-0 mechi ya kwanza nyumbani England watakuwa wageni wa Lille Uwanja wa Stade Pierre-Mauroy Jijini Villeneuve d'Ascq na Juventus baada ya sare ya 1-1 ugenini Hispania leo watakuwa wenyeji wa Juventus Uwanja wa Allianz Jijini Torino, Italia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YATUPWA NJE LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top