• HABARI MPYA

  Tuesday, March 01, 2022

  AZAM FC YATOA SARE 0-0 NA COASTAL CHAMAZI


  WENYEJI, Azam FC wamelazimishwa sare ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Kwa sare hiyo, Azam FC inafikisha pointi 25 katika mchezo wa 16 na kuendelea kushika nafasi ya tatu, ikizidiwa pointi sita na mabingwa watetezi, Simba yenye mechi moja mkononi, ikiwa nyuma ya Yanga yenye pointi  42 za mechi 16 pia.
  Coastal Union kwa upande wao wanafikisha pointi 18 katika mchezo wa 16 pia sasa wakiwa nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YATOA SARE 0-0 NA COASTAL CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top