• HABARI MPYA

  Sunday, March 06, 2022

  MAYELE AING’ARISHA YANGA MBELE YA GEITA KIRUMBA


  BAO pekee la mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele limetosha kuiongezea Yanga pointi tatu katika vita ya ubingwa wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ndani ya miaka mitano.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, Mayele aliye katika msimu wake wa kwanza Yanga tangu asajiliwe kutoka AS Vita ya kwao, Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alifunga bao hilo sekunde ya 33 dakika ya kwanza.
  Kwa ushindi huo wa 1-0 ugenini, Yanga inafikisha pointi 45 katika mchezo wa 17 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 11 zaidi ya mabingwa watetezi, Simba ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi.
  Geita Gold baada ya kipigo cha leo wanabaki na pointi zao 21 za mechi 17 sasa katika nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE AING’ARISHA YANGA MBELE YA GEITA KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top