• HABARI MPYA

  Wednesday, March 23, 2022

  STARS YANG’ARA, YAICHAPA CAR 3-1


  TIMU ya Taifa ya Tanzania imepata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) katika mchezo wa kirafiki usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Taifa Stars yamefungwa na kiungo Novatus Dismas Miroshi, wa Beitar Tel Aviv Bat Yam FC ya Israel dakika ya 10 na washambuliaji, Nahodha Mbwana Ally Samatta wa Royal Antwerp ya Ubelgiji dakika ya 63 na George Mpole Mwaigomole wa Geita Gold ya nyumbani dakika ya 90 na ushei.
  Bao pekee la Jamhuri ya Afrika ya Kati limefungwa na mshambuliaji wa Gasogi United  ya Rwanda, Christian-Theodor Yawanendji-Malipangou kwa penalti dakika ya 66.
  Stars iliyo chini ya kocha Mdenmark, Kim Poulsen itacheza mechi mbili zaidi katika kalenda hii ya FIFA, nyingine dhidi ya Botawana Jumamosi na dhidi ya Sudan Machi 29, zote Uwanja wa Benjamin Mkapa pia.
  Nazo CAR na Sudan zitamenyana Jumamosi.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STARS YANG’ARA, YAICHAPA CAR 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top