• HABARI MPYA

  Monday, September 06, 2021

  YANGA YASHINDA MECHI YA PILI MFULULIZO KIGAMBONI

  VIGOGO Yanga SC jana wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Pan Africans katika mchezo wa kirafiki kwenye kambi yao, Avic Town, Somangira, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Katika mchezo ambao ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya kwanza Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United Jumamosi ijayo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, bao pekee la Yanga lilifungwa na mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele.
  Baada ya mchezo wa Jumamosi Dar es Salaam, Yanga itasafiri kwa ajili ya mechi marudiano Septemba 19 Uwanja wa Adokiye Amiesimaka Jijini Port Harcourt, Nigeria.


  Huo ulikuwa mchezo wa tatu katika maandalizi yake baada ya kufungwa 2-1 na Zanaco ya Zambia wiki iliyopita katika tamasha la Kilele cha Wiki ya Mwananchi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Na Alhamisi waliibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Friends Rangers ya Manzese hapo hapo Avic Town – mabao yake yakifungwa na washambuliaji, Mkongo Fiston Kalala Mayele na wazawa Ditram Nchimbi na Yussuf Athumani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YASHINDA MECHI YA PILI MFULULIZO KIGAMBONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top