• HABARI MPYA

  Friday, September 03, 2021

  YANGA SC YASHINDA 3-1 MECHI YA KIRAFIKI KIGAMBONI


  TIMU ya Yanga SC jana imecheza mechi ya kirafiki kambini kwao, Avic Town, Somangira, Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Friends Rangers ya Manzese. 
  Mabao ya Yanga SC inayojiandaa na mchezo wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United ya Nigeria wiki ijayo hapa Dar es Salaam yalifungwa na washambuliaji, Mkongo Fiston Kalala Mayele na wazawa Ditram Nchimbi na Yussuf Athumani.
  Yanga SC watakuwa wenye wa Rivers United Septemba 12 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa kabla ya timu hizo kurudiana Septemba 19 Uwanja wa Adokiye Amiesimaka Jijini Port Harcourt.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YASHINDA 3-1 MECHI YA KIRAFIKI KIGAMBONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top