• HABARI MPYA

  Thursday, September 02, 2021

  TAIFA STARS YALAZIMISHA SARE 1-1 NA DRC KWAO

   
  TANZANIA imelazimisha sare ya 1-1 na wenyeji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo wa kwanza wa Kundi J kufuzu Kombe la Dunia mwakani nchini Qatar.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa TP Mazembe Jijini Lubumbashi, wenyeji The Leopard 'Chui' walitangulia kwa bao la mshambuliaji wa Kuwait SC ya Kuwait, Dieudonné "Dieumerci" Mbokani Bezua dakika ya 23, kabla ya kiungo mshambuliaji wa Wydad Athletic ya Morocco, Simon Happygod Msuva kuisawazishia Taifa Stars dakika ya 35.
  Kipindi cha pili kilikuwa cha mashambulizi ya pande zote mbili, lakini ngome za timu zote mbili zikasimama imara kutoruhusu mabao zaidi.
  Mechi nyingine ya Kundi J inaendelea hivi sasa baina ya wenyeji, Madagascar na Benin. Mechi zijazo Septemba 7 Tanzania watakuwa wenyeji wa Madagascar na Benin watakuwa wenyeji wa DRC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YALAZIMISHA SARE 1-1 NA DRC KWAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top